Jumamosi 28 Juni 2025 - 13:45
Makombora ya Iran ni sawa na jinamizi kwa Wazayuni

Hawza/ Sayyid Abdulmalik Badruddin al-Houthi, ametoa pongezi kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutokana na ushindi wake katika vita vilivyoanzishwa kwa kulazimishwa na utawala dhalimu wa Kizayuni, na akaongeza kuwa: Vita hivi vilikuwa ni sawa na jinamizi la kweli kwa uwepo wa utawala wa Kizayuni!

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Kiongozi wa Ansarullah Yemen, katika hotuba yake ya televisheni alisema: Ushindi wa Iran ni ushindi wa ulimwengu mzima wa Kiislamu, tunaitakia Iran na Waislamu wa dunia nzima pongezi kwa ushindi huu.

Lengo la Israel katika hujuma hii lilikuwa ni kuiangamiza Jamhuri ya Kiislamu, lakini mpango huo umeshindwa kabisa, hwa hakika si Israel muharibifu peke yake iliyoshindwa, bali pia kundi la waasi linaloongozwa na Marekani kwa kushirikiana na Uingereza, Ujerumani na Ufaransa limedhalilika kwa fedheha ya kushindwa huku, tumeona kwamba katika vita hivi, Waisraeli nao walipitia hali ya kushambuliwa kwa mabomu kama ile wanayoipitia Wapalestina.

Abdulmalik al-Houthi aliongeza kuwa: Israel kwa kweli imepata kipigo kikali, ilhali Iran, kwa baraka ya kiongozi mwenye nguvu, taifa lililo na mshikamano, Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi na jeshi makini, ilikuwa mshindi katika vita hivi.
Alionya kuwa; lengo kuu la mashambulizi dhidi ya Iran lilikuwa ni kubadili sura ya Asia ya Magharibi, na hili lina maana kuwa maadui bado wanataka kubadili tawala na nchi nyingine katika eneo letu na hawataacha uadui wao dhidi yetu.

Mwisho, alisema kuwa: Hii ni neema ya Mwenyezi Mungu kwamba utawala huu dhalimu, licha ya kumiliki silaha na kusaidiwa na Marekani, haukuweza kushinda vita hivi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha